The House of Favourite Newspapers

Watoto 3,524 Wamebakwa, 637 Wamelawitiwa, 130 Wamechomwa Moto

0

Jumla ya watoto 6,168 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia kati ya Januari hadi Desemba 2021, Bunge limeelezwa leo Ijumaa Novemba 12, 2021. Kati ya hao, watoto wa kike walikuwa 5,287 na wanaume ni 881 ambao kesi zao zikiripotiwa katika vituo vya Polisi nchini.

 

Takwimu hizo zimetolewa bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamisi Hamza Chilo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Ester Matiko.

 

Katika maswali ya msingi Matiko ametaka kujua ni watoto wangapi wamefanyiwa ukatili huo kwa jinsia zao wa kike na wa kiume na wangapi wamepata mimba.

 

Mbunge huyo amehoji kuhusu takwimu halisi ya hatua zilizo chukuliwa na Serikali dhidi ya matukio hayo. Chilo amesema watoto waliobakwa wapo 3,524, ulawiti ni watoto 637 wanaume wakiwa 567 na watoto wa kike wapo 70.

 

“Ukatili kwa watoto umekithiri kama vile ubakaji, ulawiti, kuchomwa moto na mimba za utotoni, je ni watoto wangapi wamefanyiwa ukatili huo? na je kuna takwimu halisi ya hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya matukio hayo?” amehoji Esther Matiko.

 

Akijibu swali hilo, Cholo amesema; “Kuanzia Januari hadi Septemba 2021 jumla ya watoto 6,168 wamefanyiwa ukatili, waliobakwa ni 3,524, waliolawitiwa ni 637, waliochomwa moto ni 130 (watoto wakiume wakiwa 33 na wakike wakiwa 97), waliopata mimba ni 1,877 na watuhumiwa waliokamatwa na kufikishwa Mahakamani ni 3,800,” amesema Chilo.

 

Kuhusu watuhumiwa amesema waliokamatwa na kufikishwa mahakamani wapo 3,800 na kesi zilizochini ya upelelezi ziko 2,368 na zilizohukumiwa ni kesi 88 wakati zingine ziko katika hatua mbalimbali katika mahakama.

Leave A Reply