The House of Favourite Newspapers

WATOTO WA KIKE WAFA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI RUSSIA

 

 

Maria Vinogradova (12) na dada yake Anastasia Svetozarova (kushoto),15, walikutwa wamekufa kwenye theluji kando ya barabara chini ya jengo walilokuwa wakiishi mjini Izhevsk, magharibi mwa Russia.
Miili ya wasichana hao ikiwa kwenye theluji (kushoto) baada ya kujitupa kutoka ghorofa ya kumi.
Maria anayesemekana alikuwa amekumbwa na mfadhaiko baada ya mama yake kukasirishwa aliposikia ameanza uhusiano wa kimapenzi na mtoto mdogo wa kiume aliyekuwa anamzidi umri.
Anastasia alirekodi video ambamo alisema: “Kwa heri wote! Nawapenda wote!! Hii ni kweli. Nawapenda sana.”
Inasemekana Maria alikuwa ameanza uhusiano na mtoto mdogo wa kiume aitwaye Dmitry (pichani).
Taswira nyingine ya miili ya wasichana hao ikiwa kwenye theluji.

POLISI wa Izhevsk, Jamhuri ya Udmurt, Russia, wanachunguza iwapo vifo vya watoto wawili wa kike waliojirusha na kufa kutoka paa ya jengo la ghorofa ya kumi vinahusiana na ‘mchezo’ ulioenea wa kujinyonga ujulikanao kama Blue Whale (Nyangumi wa Bluu).

Maria Vinogradova  mwenye umri wa miaka 12 na dada yake Anastasia Svetozarova (15) walikutwa wamekufa kando ya barabara chini ya jengo walilokuwa wakiishi mjini Izhevsk, ikiaminika walijirusha kutoka katika paa la jengo la  ghorofa ya kumi.

 

Maria anasemekana alikuwa amekumbwa na mfadhaiko pale  mama yake alipompeleka kwa mtaalam wa masuala ya uzazi baada ya kudaiwa kwamba alikuwa ameanza uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa kiume aliyekuwa na umri mdogo aliyejulikana kama Dmitry.  Mama huyo alikuwa amechukizwa vibaya ya jambo hilo.

 

Vilevile, Anastazia naye alisemekana kuwa alikuwa amekumbwa na mfadhaiko uliotokana na jambo ambalo halikufahamika.

 

Mamia ya watoto na vijana chini ya umri wa miaka 20 wanahofiwa kujiua mnamo miaka ya karibuni baada ya kulishwa kasumba katika mitandao kukamilisha kile kiitwacho hatua 50 ambazo hatimaye huelekea katika kujiua.

 

Blue Whale na magenge mengine yenye kuchochea vifo katika mitandao yanasemwa na polisi kuwalenga vijana wenye matatizo na mifadhaiko.

 

Katika uchunguzi huo, polisi wanachunguza simu na kompyuta za watoto hao wa kike ili kugundua iwapo kuna alama zozote ambazo makundi yenye kuchochea vifo yalizitumia kuwafanya wasichana hao wajitoe uhai wao.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

 

Comments are closed.