Watu 13 Wafariki kwenye ajali ya barabarani Pakistan, 14 Wajeruhiwa
Maafisa wa Pakistan wamesema kwamba takriban watu 13 wameuwawa na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea kwenye barabara kuu ya Multan Sukkur Gondal Ijumaa usiku.
Mkuu wa polisi wa wilaya, Rizwan Umar ameuambia mtandao mmoja wa habari wa Pakistan wa Dawn.com, kwamba basi la abiria lilisimama ili kuwasaidia watu waliokuwa wamepata ajali katika gari lililokuwa limepinduka.
Wakati abiria wa basi hilo walipokuwa wakitoa msaada, gari jingine aina ya Jeep liligonga basi lao la kusababisha maafa hayo. Ajali za barabarani nchini Pakistan mara nyingi hutokea kutokana na kutotii sheria barabarani, na kupelekea vifo vya maelfu ya watu pamoja na majeruhi kila mwaka.