The House of Favourite Newspapers

Watu Zaidi ya 920 Wafariki Dunia Kutokana na Kimbunga Nchini Afghanistan

0
Tetemeko lililotokea nchini Afghanistan

ZAIDI ya watu 920 wanasadikiwa kufariki katika nchi ya Afghanistan nje kidogo ya Kusini Mashariki mwa mji uliokaribu na mpaka wa Pakistan kutokana na tetemeko kubwa la ardhi.

 

Katika tetemeko hilo lililokuwa na magnitude 6.1 limeacha majeruhi wengine 200 huku vifo vingi vikithibitishwa kutokea katika Jimbo la Paktika ambapo watu 255 walifariki hiyo ni kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Ndani Salahuddin Ayubi.

Madhara ya tetemeko la ardhi Afghanistan

Katika Jimbo la Khost imeripotiwa vifo vya watu 25 huku wengine 90 wakipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu kama majeruhi.

“Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya maeneo kuwa katika mazingira magumu kufikika huku yakiwa na asili ya milima na itachukua muda mrefu kuweza kufika na kupata taarifa katika maeneo hayo.”

watu 300 wameripotiwa kufariki katika janga hilo la tetemeko

Janga hilo limeibuka wakati mabo Aghanistan inapitia kipindi kigumu cha anguko la uchumi katika nchi hiyo tangu Taliban wakamate dola mwezi Agosti mwaka jana.

 

Tangu kutawazwa kwa utawala wa Taliban Serikali nyingi zimeweka vikwazo kwenye sekta ya Benki kwa taifa hilo na kusababisha kupotea kwa mabilioni ya pesa za misaada kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya nchi hiyo.

Leave A Reply