The House of Favourite Newspapers

Watu Nane Wakamatwa kwa Kutofunga Mwezi Mtukufu

0

 

WATU nane wamekamatwa na polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria  kwa madai ya kukataa kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 

Polisi wa Hisbah wanasimamia sheria za Kiislam huko Kano – moja ya majimbo 12 ya Waislamu kaskazini mwa Nigeria wanaotumia mfumo wa sheria wa Sharia pamoja na sheria za kidunia za nchi hiyo.

 

“Waliokamatwa walikuwa wanawake watano na wanaume watatu, wakila mchana katika mwezi wa Ramadhan,” Aliyu Kibiya, Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Hisbah Jimbo la Kano alinukuliwa akisema.

 

Kufunga kwa watu wazima ni suala la wajibu hasa kwa wale wenye uwezo wa kutokula na kunywa.

 

Walio wagonjwa na wale ambao wanaweza kupata athari za kiafya iwapo watafunga kula na kunywa, wakiwemo watoto, wanawake wajawazito, wasafiri na wanawake wanaonyonyesha.

 

Kwa mujibu wa BBC wanawake hao waliiambia Hisbah kwamba walikuwa na msamaha kwa kuwa wako kwenye hedhi, lakini polisi waliwaambia pamoja na hali hiyo hawakupaswa kula hadharani.

 

Ikiwa watashtakiwa mahakamani, wanaweza kulipishwa faini au kupelekwa kwa taasisi ya marekebisho ya tabia.

 

Taarifa ya Kibiya ilionya kuwa uvamizi zaidi utafanywa katika jimbo lote kuhakikisha watu wanazingatia wajibu wao wa kidini.

 

Leave A Reply