The House of Favourite Newspapers

Watu Zaidi ya 150 wauawa katika mashambulizi Paris, Ufaransa

0

Rue BichatMauaji katika mghahawa wa Rue Bichat, ParisAmbulance Gari la huduma ya kwanza.BataclanWalionusulika katika shambulizi lililofamyika kwenye ukumbi wa Batclan.
Batclann …Wakiokolewa.Cambodian Miili ya marehemu  katika mhgahawa wa Cambodian.Paris Hali ya sintofahamu mjini paris.ParissKikosi cha uokoaji.Parisss

…Mmoja wa waliouawa baada ya kukutwa eneo la Boulevard des Filles du Calvaire karibu na Btclan, Paris.doriamajeruhi
okoa …Wakiokolewa.polisi doriaPolisi wakikagua vitambulisho vya raia wakati wa doria.ramaniEneo amabapo mashambulizi hayo yamefanyikauwanja uwanja2

Hali ilivyokuwa uwanja wa michezo wa Ufaransa, Stade de France

Paris, Ufaransa

UFARANSA imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 150 kuuawa kwenye mashambulio mjini Paris, usiku wa kuamkia leo.

Watu 118 wameuawa baada ya kuvamiwa, kutekwa na baadaye kufyatuliwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wapiganaji wa IS katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa Mji wa Paris wakati walipokuwa wakitazama tamasha.

Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla ya maofisa wa polisi kufika meneo la tukio na kupambana nao na kuwazidi nguvu.

Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa hilo, Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.

Viongozi wa Mji wa Paris wamewataka raia kubaki majumbani mwao wakati wanajeshi 1500 wa nchi hiyo wameingia katika mitaa mbalimbali ya mji wa Paris kufanya doria kuwasaka wahusika wa mashambulizi hayo.

Shambulio baya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.

Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa “bila huruma”.

Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge watu wapatao 11 wameuawa Rue Bichat, Cambodian, na Le Carillon katika mtaa namba 10.

Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa “jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia” na kuahidi kuisaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.

“Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja,” amesema.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya “lolote tunaloweza kufanya kusaidia.”

Leave A Reply