The House of Favourite Newspapers

Bella, Kiba Waunda Bongodansi

0

christian bellaaMkali wa dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella.

MUSA MATEJA

MKALI wa dansi mwenye asili ya Kongo, Christian Bella amefunguka kuwa anajivunia mafanikio makubwa waliyoyapata baada ya kufanikiwa kuingia studio na mkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba kuzalisha wimbo mkali ambao umeleta ladha ya Dansi na Bongo Fleva, BongoDansi.

kibaMkali wa Bongo Fleva, Ali Kiba

Akizungumza na gazeti hili, meneja wa Bella aliyejitambulisha kwa jina la Simple, alisema Bella na Kiba wamefanya ngoma hiyo kubwa kwenye Studio za Chedaz Record zilizopo Mikocheni jijini Dar chini ya prodyuza Abidady ukiwa ni utunzi wa Christian Bella.

Alisema wimbo huo ambao una ladha kali kutoka kwa wasanii hao wakali wa Dansi na Bongo Fleva, tayari umeshakamilika na wameshaufanyia video ambayo wameifanyia jijini Nairobi Kenya kwa Director Enock. “Lengo ni kuleta kitu cha tofauti kwa mashabiki.

Wimbo unakwenda kwa jina la Nagha-limia, tayari umeshaingia kwenye vituo mbalimbali vya redio, utambulisho wa audio ataufanya Ali Kiba kwani Bella yuko kwao Kongo kwenye matatizo ya kifamilia. Anatarajia kurejea siku chache zijazo na akifika tu atafanya kazi ya kuachia video,” alisema Simple.

Leave A Reply