The House of Favourite Newspapers

Watu Zaidi ya 20 Mbaroni Oparesheni ya Kusaka Majambazi Vikindu

0

Kamanda SirroJeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limewakamata zaidi ya watu 20 ambao kati yao wanahusishwa na tukio la mauaji ya askari polisi 4 lililotokea siku za hivi karibuni maeneo ya Mbande, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano, jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo Kamanda Simon Sirro alisema kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Operesheni inapata mafanikio makubwa tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu zaidi ya 20 maeneo ya vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio mbalimbali ikiwemo lile la mauaji, ” amesema.

Aidha, Kamanda Sirro amewashukuru viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha operesheni Ukuta waliyoipanga kuifanya kesho.

“Niwapongeze kwa maamuzi ya busara waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie tu kwamba Dar es Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa wasiogope watakapo waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya doria ili jiji liwe salama, ” amesema.

Pia amesema Viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe na Edward Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho Katika kituo hicho, wanatakiwa kuripoti siku ya jumanne ya wiki ijayo.Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limewakamata zaidi ya watu 20 ambao kati yao wanahusishwa na tukio la mauaji ya askari polisi 4 lililotokea siku za hivi karibuni maeneo ya Mbande, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda hiyo Kamanda Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na jeshi hilo maeneo ya Vikindu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

“Operesheni inapata mafanikio makubwa tangu ilipoanza na kwamba tumewakamata watu zaidi ya 20 maeneo ya vikindu na Dar es Salaam wakihusishwa na matukio mbalimbali ikiwemo lile la mauaji, ” amesema.

Aidha, Kamanda Sirro amewashukuru viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuaghirisha operesheni Ukuta waliyoipanga kuifanya kesho.

“Niwapongeze kwa maamuzi ya busara waliyofanya maana ni ya kizalendo, niwahakikishie tu kwamba Dar es Salaam iko salama na pia niwatoe hofu wananchi kuwa wasiogope watakapo waona askari barabarani sababu kazi yao ni kufanya doria ili jiji liwe salama, ” amesema.

Pia amesema Viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa Freeman Mbowe na Edward Lowassa waliotakiwa kuripoti kesho Katika kituo hicho, wanatakiwa kuripoti siku ya jumanne ya wiki ijayo.

Leave A Reply