The House of Favourite Newspapers

Watumishi Watano Tanesco Walilipwa Dola 34,623 Kusafiri Bila Kibali

0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema ukaguzi uliofanywa na ofisi yake umebaini kuwa watumishi watano wa TANESCO walilipwa dola za Marekani 34,623 (takribani shilingi milioni 89.3) na kusafiri nje ya nchi bila kupata kibali cha kusafiri.

Amesema suala hilo ni kinyume cha sheria na Aya Na.1 ya Mwongozo wa Utumiaji wa Mfumo wa Vibali vya Kusafiri toleo Na. 1 la mwaka 2016 na hali hii ilisababishwa na mapungufu ya udhibiti wa ndani unaoruhusu malipo ya posho ya kujikimu kwa safari za nje bila kibali cha kusafiri kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

CAG ametoa mapendekezo kwa TANESCO iimarishe udhibiti wa ndani ili kuhakikisha watumishi wote wanaosafiri nje ya nchi kwa malengo binafsi au ya kikazi wanakuwa na kibali cha kusafiri kutoka kwa Katibu Mkuu

”MSIMKATIE SIMBA TAMAA – ANAWEZA KUWA BINGWA – HATUTAKUWA BINGWA kwa KUMFUNGA GOLI 100” – KAMWE…

Leave A Reply