The House of Favourite Newspapers

Hizi Hapa Sababu za ATCL Kupata Hasara ya shilingi bilioni 56.64

0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amesema ukaguzi uliofanywa na ofisi yake umebaini Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeendelea kupata hasara kwa miaka sita mfululizo.

Mwaka wa fedha wa 2022/23 ATCL ilipata hasara ya shilingi bilioni 56.64 ikiwa imeongezeka ikilinganishwa
na hasara ya shilingi bilioni 35.23 mwaka wa 2021/22 na kwamba ATCL imeendelea kupata hasara licha ya kuwa inapokea ruzuku kutoka Serikalini.

Kichere amesema sababu zinazopelekea hasara zinajumuisha kuwapo kwa gharama kubwa za uendeshaji wa shughuli za ATCL, pamoja na gharama zisizoepukika kama vile gharama za ukodishaji na bima kwa ndege ya Airbus A220 -300 isiyofanya kazi kutokana na matatizo ya kiufundi kama vile kutu na kasoro za injini.

Matatizo haya yamegunduliwa na mtengenezaji wa ndege hiyo na yameathiri idadi ya ndege za aina hi kote ulimwenguni.

Kuharibika kwa ndege ya Airbus A220 – 300 kuliathiri mwenendo wa safari za ndege, hivyo kusababisha ATCL kukosa mapato na kushindwa kufidia gharama za kudumu za ndege iliyoharibika.

Aidha, Serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuboresha uendeshaji wa ATCL ikiwemo kuundwa kwa timu ya wataalamu inayofanya tathmini ya masuala ya kiufundi ya ndege, kifedha na utendaji wa ATCL katika biashara ya usafiri wa anga.

Leave A Reply