WATUMISHI wawili wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tanzania Rural and Urban Road Agency – TARURA) wamefariki dunia na wengine watatu wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea Izazi katika Barabara Kuu ya Iringa-Dodoma baada ya gari lao kugongana na lori lililohama upande baada ya kumshinda dereva wake.
TAARIFA YA POLISI
Mnamo tarehe 25.06.2019 majira ya 05:45 hrs maeneo ya Izazi kata ya Izazi tarafa ya Ismani wilaya ya Iringa na mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Iringa-Dodoma.
Gari lenye namba za usajili STL 3807 aina ya Toyota Hilux, mali ya TARURA, likiendeshwa na Lodrick s/o Richard@Ulio, miaka 35, kabila Mchaga na mkazi wa DSM likitokea Iringa kuelekea Dodoma liligongana uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T 146 BAZ aina ya Mitsubish Fuso mali ya Wilson S/o Msenga wa Iringa likiendeshwa na Amos s/o ??? wa Iringa likitokea Dodoma kuelekea Iringa.
Madhara
VIFO
1. Lodrick s/o Richard@Ulio-dereva wa TARURA
2. Joyce d/o Enezar@Mlay, miaka 45, kabila Mchagga mkazi wa Moshi.
MAJERUHI
1. Ernest s/o Mgeni, miaka 49, kabila mkinga na mkazi Mbozi
2. Gervas s/o Myovela, miaka 44, kabila mhehe mkazi wa Mbozi
3. Jamadin s/ Mikata, miaka 32, kabila mngoni na mkazi wa Mbozi
Wote walikuwa kwenye gari la TARURA na wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Iringa kwa matibabu.
Aidha, miili ya marehemu imekabidhiwa kwa meneja wa TARURA manispaa Iringa na kupekekwa Dodoma tayari kwa utaratibu wa mazishi.
Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa Fuso kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha kuhama upande mmoja na kugongana uso kwa uso ambaye amekimbia mara baada ya ajali hiyo na anatafutwa.
WITO
Madereva wawe makini wanapotumia barabara wasijione wako peke yao bali waheshimu sheria na watumiaji wengine wa barabara.
Comments are closed.