The House of Favourite Newspapers

Rostam Afunguka Kilichomrudisha Nchini, Amtaja Magufuli- Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz alipowasili kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Ltd. mfanyabiashara Rostam Aziz, amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuweka usawa wa kibiashara katika miaka minne ya uongozi wake.
Aidha, mfanyabiashara huo ameahidi kuwekeza katika miradi mingine zaidi nchini itakayogharimu zaidi ya Sh bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz kuangalia Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo kabla ya kuvizindua huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
Rostam amesema hayo leo Jumanne Juni 25, Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ghala na mitambo ya gesi ya taifa (Taifa Gas) ambayo ni gesi ya majumbani iliyozinduliwa rasmi na Magufuli.
Amesema mafanikio ambayo wao kama Taifa Gas na makampuni mengine kutoka nje wanayaona yanatokana na kazi kubwa aliyoifanya Magufuli tangu aingie madarakani mwaka 2015.
Rais Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Ghala na Mitambo ya kuchakata Gesi ya LPG vya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
“Uimarishwaji wa sekta binafsi utatekelezwa kwa uwanja ulio sawa kama kujenga miundombinu itakayowasaida Watanzania kujikwamua kutoka katika umaskini wa kihistoria na mheshimiwa Rais historia itakukumbuka katika hili,” amesema Rostam.
Rais Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
“Kuna watu walisema kuwa wewe si rafiki wa sekta binafsi,  nataka niwaambie kuwa uongozi wako ndiyo umefanya nianze kurudisha mitaji ya uwekezaji ambayo niliwekeza nje, na Taifa Gas ni mwanzo tu ila kuna miradi mingine itakayogharimu Sh. bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo,” amesema.
Rais Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz baada ya kuzindua Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG.

JPM, ROSTAM AZIZ KATIKA UZINDUZI WA GHALA KIGAMBONI

Comments are closed.