The House of Favourite Newspapers

Wauza sukari wamhujumu Rais Magufuli

0

Sukari-001Sukari.

Stori: Makongoro Oging’, UWAZI

DAR ES SALAAM: Upatikanaji wa sukari nchini kwa bei ya Sh. 1,800 iliyotangazwa na serikali bado ni ndoto na kwa sasa wafanyabiashara wakubwa wanaosambaza bidhaa hiyo wamegoma kushusha bei, baadhi wenye bidhaa hiyo ghalani wanaficha kwa madai kuwa, bei hiyo hailipi.

SONY DSC

Wakaguzi kutoka ofisi ya Rais (Mipango) wakiwa naviongozi wa kiwanda cha Sukari Kagera.

Baadhi ya wananchi waliohojiwa na Uwazi kwa njia ya simu kutoka mikoa mbalimbali wamedai kuwa, bei ya sukari mpaka sasa katika maeneo mengi nchini ni kati ya Sh. 2,000 hadi 2, 400 kwa kilo hali ambayo wanaitafakari kuwa ni kumhujumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwani haiwezekani bei mpya ya sukari isitumike wakati ni tamko la serikali.

Wananchi wengi waliendelea kuhoji iweje serikali ikae kimya wakati sukari nyingi wamekuwa wakiiona kwenye maghala ya serikali ambapo haisambazwi kutokana na mgomo wa wafanyabiashara wakubwa?
“Tulifurahi sana tuliposikia rais akitangaza sukari isitoke nje ya nchi badala yake itumike inayozalishwa nchini kwani inatosheleza lakini matokeo yake upatikanaji wake umekuwa mgumu.

Charles_MwijageWaziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage.

“Serikali imekaa kimya pamoja na waziri anayehusika. Inaonekana hawana meno kabisa kwani wanashindwa kuilinda bei mpya walioitangaza wakati polisi na vyombo vingine vya usalama vipo. Wangeamriwa kufanya msako mkali kwa wale waliogoma na kuficha bidhaa hiyo na kama ikiwezekana wanyang’anywe leseni ili iwe fundisho,” alisema Jane Wambura wa Kitunda, Dar.

Baadhi ya waandishi wetu mikoani waliohojiwa kuhusiana na bei ya sukari katika maeneo yao walikuwa na haya ya kusema:
Mkoa wa Mwanza (kilo shilingi 2,000 hadi 2,200), Arusha (2,000), Mara (2,000 hadi 2,400), Tanga (2,000), Pwani (2,000), Morogoro (2,000), Iringa (2,000 hadi 2,200), Tabora (2,000), Kigoma (2,200), Lindi (2,000 hadi 2,200), Kagera (2,000) na Kilimajaro (2,000). Dar es Saalam ni Sh. 2,000 hadi 2,200.
Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwanza alitangaza na kuagiza bei ya sukari ishushwe kwa kilo moja kuwa Sh. 1,800 katika maduka yote lakini wapi.

Magufuli amalizia Baraza la Mawaziri-001Rais Magufuli.

Ukiachana na mkurugenzi huyo, Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage naye alikuja na tamko lake ya kumridhisha Rais Magufuli kwa kutangaza kuwa, wanaopandisha bei baada ya rais kutangaza ni wahujumu uchumi na watakaobainika watafutiwa leseni ya biashara lakini mpaka sasa hakuna aliyefutiwa wala kufikishwa mahakamani.
Juzi, gazeti hili lilimtafuta Waziri Mwijage na kumpata kwa njia ya simu ambapo alipoulizwa kuhusu hali hiyo, alisema:
“Niko kanisani, hivi hapa nimetoka nje ili kupokea simu yako,” akakata.

Leave A Reply