The House of Favourite Newspapers

Wavuvi Watatu Wapigwa Risasi

0
Faki Mbaruku.

UMATI wa wavuvi kupitia chama chao cha Wavuvi Wadogowadogo Minazi Mikinda (WAWAMI) wa jijini Dar es Salaam, wameicharukia serikali baada ya mwenzao mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Masudi kudaiwa kupigwa risasi baharini akiwa kwenye shughuli za uvuvi.

Wavuvi walicharuka zaidi baada ya kuambiwa mwenzao huyo alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na gari la wagonjwa la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Mizinga kilichopo Kigamboni.

 

Wavuvi wakiendelea na kikao.

 

Akizungumza na Uwazi, Mwenyekiti wa WAWAMI, Kai Ally alisema taarifa alizozipata kutoka kwa wavuvi waliokuwa na marehemu walimwambia wakiwa kwenye mwambao, walijitokeza watu wenye silaha na kuwaweka chini ya ulinzi na kuwaambia kuwa walikuwa kwenye oparesheni ya kusaka wavuvi haramu.

 

Juma Mwingano.

 

Baada ya kuambiwa hivyo walitii amri na kuongozwa na watu hao mpaka kando ya bahari lakini ilitokea hali ya kutoelewana hivyo wavuvi wengine pamoja na marehemu waliondoa vyombo vyao vya uvuvi na kuanza kutimka kila mmoja na njia yake.

Kai alidai katika hali hiyo watu hao walianza kuwafyatulia risasi ambazo ziliwapiga wavuvi watatu ambao waliwataja kuwa ni Ally Madaba, Juma Juma na Juma Masudi ambaye alifariki muda mfupi baadaye.

 

Dotto Msawa.

 

“Tunaiomba serikali iwasake wauaji hao na hata kama walikuwa katika doria za kuwasaka wavuvi haramu, haikuwa busara kuwapiga risasi na kuwaua kwa kuwa kitendo hicho ni kuwahukumu kifo bila kuwafikisha mahakamani. Isitoshe hayo ni matumizi mabaya ya silaha,” alisema Kai.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Salum Hamduni alipopigiwa simu mara kadhaa na Uwazi ili atolee ufafanuzi sakata hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.

 

Majadiriano yakiendelea.

 

Baada ya kamanda huyo kutopatikana gazeti lilimtafuta Diwani wa Kata Kigamboni, Dotto Msawa ambaye alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema analifuatilia kwa karibu na atalitolea ufafanuzi hapo baadaye kwa kuwa anashirikiana na viongozi akiwemo Faki Mbaruku na Mwenyekiti wa Mtaa wa Feri, Juma Mwingano aliyekuwepo kwenye kikao hicho

 

Juma Masoud enzi za uhai wake.

Diwani huyo aliongeza kuwa marehemu huyo amezikwa juzi Jumapili ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwa kaka yake marehemu huko Yombo Buza jijini na uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vya dola.

STORI: Richard Bukos na Issa Mnally | UWAZI| Dar

 

Wavuvi Walilia Maiti ya Ndugu Yao

Leave A Reply