The House of Favourite Newspapers

Wawa: Corona Siyo Ya Kuchukulia Utani

0

BEKI kisiki wa Simba, Pascal Wawa, amesema kuwa Virusi vya Corona siyo vya kuchukulia utani, ni lazima kila mmoja achukue tahadhari.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Wawa alisema kuwa kwa sasa anafanyia mazoezi ndani kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.

 

“Nipo nyumbani na hali bado haijawa nzuri kwa sasa tunaomba Mungu mambo yarudi kama zamani kwani kwa sasa ninafanyia mazoezi nyumbani, hivyo ni lazima tuchukue tahadhari kuhusu Corona,” alisema Wawa.

 

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitoa tamko hilo Machi 17.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka

Leave A Reply