The House of Favourite Newspapers

Wawili Wafariki kwa Corona Iran

0

SERIKALI ya Iran imethibitisha vifo vya watu wawili vilivyotokana na maambukizi mapya ya virusi vya Corona na kuvifanya kuwa vifo vya kwanza kuripotiwa eneo la Mashariki ya Kati. Maafisa wa afya nchini Iran, wamesema wanaume wawili wazee wamefariki dunia katika mji wa Qom.

 

Shirika la habari la Iran IRNA, limesema shule na vyuo huenda vikafungwa katika mji huo wa Qom kwa ajili ya kufanya uchunguzi. Kwingineko watu tisa wameripotiwa kuwa na maambukizi ya Corona katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

 

China imeripoti kuendelea kupungua kwa kasi ya maambukizi hii leo na kuweka matumaini ya kumalizika kwa mripuko huo, huku Japan ikikosolewa kutokana na abiria wawili waliokuwamo ndani ya meli iliyowekwa chini ya karantini kufariki.

 

Idadi ya vifo ndani ya China bara imefikia watu 2,118 baada ya watu wengine 114 kufariki dunia. Zaidi ya watu 74,000 wameambukizwa virusi hivyo ndani ya China na mamia wengine katika nchi zaidi ya 25.

Leave A Reply