The House of Favourite Newspapers

Waziri Biteko Akagua Wauza Madini Dar, Aonya Matapeli

0
Waziri wa Madini, Dotto Biteko (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa madini alipotembelea na kukagua vizimba vya wafanyabiashara hao vilivyopo katika Soko la madini la mikoa ya Pwani na Dar es Saaam lililopo katika Jengo la NHC Barabara ya Samora jijini Dar. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukuru Manya.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewacharukia matapeli wanaojihusisha biashara ya uuzaji na ununuzi wa madini kinyemela  majumbani mwao na kuikosesha serikali mapato na kuongeza kuwa huo ni uhalifu ambao kamwe  hautavumiliwa.

Waziri Biteko pia amewaonya matapeli wanaowalaghai wageni kutoka nje ya nchi na kuwauzia madini feki jambo alilosema linachafua sifa ya nchi.

Makamu Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara Wakubwa Wanunuzi na Wauzaji Madini Tanzania (TAMIDA), Osman Tharia akizungumzia katika mkutano huo uliofanyika baada ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko kutembelea vizimba vya wafanyabiashara hao.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo leo alipotembelea na kuwakagua wafanyabiashara wa madini kwenye soko la madini lililopo Jengo la NHC Barabara ya Samora jijini Dar ambapo alisikiliza changamoto zinazowakabili wadau hao na kuahidi kuzitatua haraka.

“Lengo letu ni kudhibiti utoroshaji wa madini ndio maana tumekuja kuwapa tahadhari kuwa wajiepushe kununua nje ya mfumo wa masoko kwani madhara yake ni makubwa. ukikutwa unanunua au unauza madini nyumbani kwako hata kama upo kwenye gorofa ya 12, fensi kali na kamera za CCTV tutakukamata.

Baadhi ya wafanyabiashara wa madini katika soko la madini Dar es Salaam na Pwani wakiwa katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam baada ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko kuwatembelea. “Lazima tufuate sheria kwa sababu asilimia saba ya pato hilo sio kubwa kiasi cha kukusababishia kwanza tutaifishe madini, nyumba na hata wewe mhusika kupelekwa ndani,” alisema.

Alisema katika kudhibiti mnyororo wa sekta ya madini, Serikali kupitia wizara ya madini pamoja na wizara ya viwanda na biashara inaandaa muswada wa sheria utakaowawezesha masonara wote nchini kutambulika kisheria.

Naibu Waziri wa Madini akizungumza katika mkutano huo baada ya kukagua vizimba vya wafanyabiashara wa madini katika soko hilo.

“Tatizo ni kubwa kwa masonara ni kutotambulika… kwa kuwa wapo wengin hata kuwatambua ni ngumu. Tunataka kuweka msukumo mkubwa zaidi katika udhibiti mifumo mingi katika sekta ya madini na sasa tumeweka mazingira rafiki kwa sababu lengo letu ni uongezaji thamani. Kikubwa nawaomba masonara wawe na subira katika hili,” alisema.

Naye Makamu Mwenyekiti Chama cha Wafanyabiashara Wakubwa Wanunuzi na Wauzaji Madini Tanzania (TAMIDA), Osman Tharia aliiomba wizara kuuangalia upya bei ya pango la vizimba walivyokodishwa na Shirika hilo la nyumba sambamba na bei za umeme kwa kuwa zinawakwamisha katika kukuza biashara ya madini nchini.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko akizungumza na wafanyabiashara hao baada ya kukagua vizimba na kujionea namna wanavyofanya biashara.

“Alisema wafanyabiashara zaidi ya 57 waliopo katika vizimba hivyo hulazimika kulipia umeme kulingana na ukubwa wa kizimba jambo ambalo ni gharama kubwa kwani ilitakiwa kulipia kulingana na matumizi ya umeme,” alisema.

Waziri wa Madini, Dotto Biteko na Naibu wake, Prof. Shukuru Manya wakijadiliana jambo katika mkutano huo.

Aidha, Naibu waziri wa madini, Prof. Shukrani Manya aliwataka wafanyabiashara wa madini kuzingatia sheria kwa kuwa serikali haina nia ya kuwadhoofisha kibiashara bali inataka kuwawezesha kukua na kufanya biashara ya madini kuwa endelevu na yenye tija kwa pande zote.

Leave A Reply