Waziri Kitwanga Naye Aikana Kampuni ya Lugumi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga.
Infosys ambayo imekanusha kuhusika katika sakata hilo imedaiwa kuwa iliisaidia kampuni ya Lugumi kupata vifaa kutoka kampuni ya Dell ya Marekani ili viweze kufungwa kwenye vituo vya polisi.
Jana, Kitwanga alisema anashangazwa kwa jinsi anavyohusishwa kwa maelezo kuwa wakati tukio hilo likitokea mwaka 2011, yeye hakuwa waziri wa wizara hiyo.
Lugumi.
Alichokizungumza Waziri Kitwanga
“Inanishangaza sana sihusiki na wala silijui hili suala la Lugumi. Wakati linatokea sikuwa waziri wa wizara hii ndiyo maana huwa sipendi na wala sitaki kuzungumza chochote kuhusu Lugumi,” alisema.
Kitwanga alifafanua kuwa baadhi ya mambo yameanza kubainika baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, licha ya kutotaka kuweka wazi kama suala la Lugumi ni miongoni mwa mambo hayo.
Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
Alichokizungumza Kamanda Kova
Jana Jumanne, Gazeti la Uwazi linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, lilichapisha habari kuhusu Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kuibuka na kusema kuwa hatambui chochote kuhusu sakata la Lugumi.
“Mimi nilikuwa nashughulika na wahalifu na Lugumi hakuwa mhalifu, siwezi kumzungumzia lolote kwa sababu mimi nimeshastaafu. Huku nilipo sipati taarifa zozote za kiofisi, nimekuwa kama samaki nje ya maji, sina nguvu zozote,” alisema kamanda huyo.
Aliongeza: “Lakini Lugumi namfahamu ila si kwa hilo sakata la vifaa vya kuchukulia alama za vidole ndugu yangu.”
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka 2013/14 ndiyo iliyofichua udhaifu huo. Utekelezwaji wa mkataba huo uliwasilishwa jana kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na mwenyekiti wake Aeshi Hilaly alisema wameanza kuupitia na watakapokamilisha wataweka kila kitu wazi.
Spika wa Bunge, Job Ndugai
Alichokizungumza Spika wa Bunge, Ndugai
Kwa upande wake Ndugai alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alisema, “Mimi sijapata taarifa zozote za Lugumi. Jambo hilo bado lipo katika kamati ya bunge.”
STORY ZILIZOPITA KUHUSU SAKATA LA LUGUMI
- Kova aibuka sakata la Lugumi
- Nyaraka za Kampuni ya Lugumi Zatua TAKUKURU
- Mkataba wa Lugumi wawa kaa la moto
- Bunge lajadili taarifa ya Mkataba wa Lugumi
SIKILIZA VIDEO YA MAHOJIANAO NA KAMPUNI YA INFOSYS