The House of Favourite Newspapers

Waziri Mahiga Abainisha Kisa cha Watanzania Kutimuliwa Msumbiji


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo.

Mahiga amesema kuwa Watanzania hao wamefukuzwa Msumbiji baada ya kubainika kuwa wanaishi nchini humo bila kuwa na pasipoti za kusafiria, vibali vya kuishi na kutofuata vigezo walivyokuwa wamepewa na mamlaka husika ya nchi hiyo.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ugeni unaotarajiwa kuwepo nchini Tanzania wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni anayetarajiwa kufanya ziara ya siku mbili ya Kitaifa nchini Februari 25 na 26, 2017.

Rais wa Visiwa va Shelisheli, Mhe. Dannu Faure naye atawasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili kuanzia Tarehe 27-28, februari mwaka huu.

Comments are closed.