The House of Favourite Newspapers

Waziri Mhagama Ashiriki Mkutano wa 109 Wa Nchi Wanachama ILO

0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akiwa pamoja na Kamishna wa Kazi Brig. Gen. Francis Mbindi wakishiriki mkutano wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao katika Ukumbi wa Mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani Mhe. Omar Zniber akifungua mkutano huo.
Baadhi ya Washiriki kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi (ILO). uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameshiriki mkutano wa 109 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) uliofanyika kwa njia ya Mtandao katika Ukumbi wa Mkutano uliopo jengo la PSSSF Jijini Dodoma.

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU 

Leave A Reply