The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkenda Atoa Rai Alumni Kushiriki Uboreshaji Shule Walizosoma

0

Haijalishi ni mwaka gani umemaliza Shule Msingi au Sekondari unayo nafasi kuchangia kuboresha shule uliyosoma.

Haya yamedhihirishwa na Alumni wa Shule ya Sekondari Darajani Mkoani kilimanjaro ambao viongozi wake baadhi ni wahitimu wa mwaka 1965. Kupitia umoja huo  wamechangia zaidi ya Shilingi Milioni 220 na kuzitumia kuboresha shule hiyo katika miundo mbinu, vifaa vya TEHAMA,  motisha kwa Walimu, Samani na kazi  nyingine za ujenzi ambazo zinaendelea.

Akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule hiyo  Prof. Estomih Mtui na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Wilson Minja Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf  Mkenda amepongeza Juhudi hizo na kueleza kuwa  serikali inatambua kazi kubwa zinazofanywa na Umoja huo na Alumni nyingine  mbalimbali  na kuwa itaendelea kushirikiana nao hususan katika kuimarisha miundo mbinu ya Shule zao ambazo nyingi ni shule kongwe.

Leave A Reply