The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Atoa Tamko Sakata La Bandari Ya Dar, Huu Hapa Msimamo Wa Serikali – “Tutajadiliana”-Video

0


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari nchini.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo Juni 28, 2023 wakati akilihutubia Bunge. “Kuhusu umiliki wa bandari, nilihakikishie Bunge lako na Wananchi kwa ujumla kwamba kupitia Sheria ya Bandari ya Mwaka 2004, Mamlaka ya Bandari Tanzania imekasimiwa haki ya kuwa Mmiliki wa maeneo yote ya bandari nchini na haina uwezo wa kutoa umiliki huo kwa kampuni yoyote”

“Wakati wote wa utekelezaji wa makubaliano hayo na mikataba itakayoingiwa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao katika eneo la mradi kama vilivyofanya katika kipindi cha miaka yote 22 ya mkataba na Mwekezahi wa awali (TICTS) aliyemaliza mkataba wake mwezi Novemba, 2022”

Leave A Reply