The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atua Kilombero Kukagua Athari zilizosababishwa na mafuriko

0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 16, 2024 amewasili Halmashauri ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro ambapo atakagua athari zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.

Pia Majaliwa atazungumza na wananchi waliothirika na mafuriko hayo na kuelekea Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo pia atakagua athari za mafuriko pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo ya Muhoro na Chimbi.

Leave A Reply