The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Majaliwa Ajibu Maswali Ya Wabunge Na Kutoa Maelekezo – Video

0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezielekeza Taasisi za Serikali ziendelee kujipanga kukabiliana na maafa kwa kushirikiana na wadau kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika Mpango wa Kujiandaa na Kukabiliana na Madhara ya El-Nino pamoja na mipango ya kisekta ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Maelekezo hayo ni miongoni mwa maelekezo 14 aliyoyatoa Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswalı ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu leo Aprili 25, 2024.

Amezitaka Kamati za Maafa za Wilaya na Mikoa ziendelee kuchukua hatua stahiki ikiwemo kutoa tahadhari kwa wananchi na kusaidia wananchi kwa wakati pindi maafa yanapojitokeza.

Leave A Reply