The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa Afariki Dunia Akipatiwa Matibabu

0

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki dunia leo, Februari 10, 2024 wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo chake zimetangazwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ambaye amesema Lowassa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo, mapafu na utumbo kujikunja ambapo alipelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu na baadaye kurejea jijini Dar es Salaam mpaka alipofikwa na mauti.

Taarifa zaidi zitakujia.

Leave A Reply