The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu New Zealand Aenda UN na Mwanaye Mchanga

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern akihutubia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa
Jacinda Ardern

AKIWA amefuatana na mwanaye mchanga na mpenzi wake katika ukumbi wa mkutano, Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern,  ametoa hotuba yake ya kwanza katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.

 

Katika tukio hilo ambalo si la kawaida, Ardern alichukua muda kidogo kucheza na mwanaye aitwaye, Neve Te Aroha, na kuongea na mpenzi wake, Clarke Gayford, kabla ya kulihutubia baraza hilo.

 

Kiongozi huyo kwa sasa anamnyonyesha bintiye huyo mwenye umri wa miezi mitatu, jambo ambalo limenonekana si la kawaida, kwani kwa kawaida angemuacha nyumbani kwa siku sita ambazo atakuwa katika mkutano huo.

Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21
Ardern (kulia) akiwa na mpenziya, Gayford na mtoto wao, Neve.

Hata hivyo, amesema mara nyingi huwa anakuwa na mtoto wake huyo hata akiwa nchini kwake, New Zealand.

Wakati Ardern akihdhuria mkutano huo, Gayford atakuwa na jukumu la kumtunza  Neve, kama ilivyoandikwa katika kadi inayotambulisha rasmi uwepo wa mtoto huyo katika ukumbi wa mkutano.

Ardern pia ameliambia gazeti la Herald nchini New Zealand kuwa atagharamia usafiri na malazi ya mpenzi wake, Gayford.

“Yuko hapa kwa ajili ya kumtunza mtoto wetu.”

Mpenzi wake Clarke Gayford,ambaye ni mtangazaji wa televisheni, kwa sasa anamsaidia jukumu la ulezi

Kiongozi huyo amerejea kazini kutoka likizo ya uzazi mapema mwezi Agosti mwaka huu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema waziri huyo ni kielelezo chema kwa taifa lake na hatua yake ya kuhudhuria mkutano huu akiwa na mwanaye ni ishara wazi kwamba hakuna mwakilishi bora zaidi kwa nchi kuliko mama mchapa kazi.

Dujarric, ameongeza kuwa viongozi wanawake duniani wanafanyiza asilimia tano, kwa hiyo wanahitaji kujisikia huru kadiri ya uwezo wao.

Comments are closed.