The House of Favourite Newspapers

Waziri Mwakyembe Azindua Mbio Za Marathon

Mratibu wa mashindano hayo, Aggrey Marealle akiwakaribisha wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon za 18 huku akitoa wito kwa Watanzania kushiriki mbio hizo.

Mgeni rasmi, Waziri Mwakyembe akisistiza jambo baada ya kusoma risala kwenye hafla hiyo.

Akizungumza katika Hoteli ya Best Western Coral Beach, Waziri Mwakyembe amewapongeza wadhamini wa mbio hizo wakiongozwa na Kilimanjaro Premium Lager waliodhamini mbio za Km 42.

Sehemu ya wageni waalikwa.

Tigo Km 21 na Grand Malt waliodhamini mbio za Km 5.
Ameendelea mashindano haya yanazidi kutia moyo sana ambapo sasa hivi yana washiriki zaidi ya 11,000 kutoka zaidi ya nchi 56 kote duniani.

“Hili ni jambo zuri sana kwa taifa kwani tunapata fedha za kigeni kutokana na matumizi yanayofanywa na wageni wakati wa mashindano hayo”. Alisema Waziri Mwakyembe.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, wadhamini wakuu wa mbio hizo, Pamela Kikuli akiongea kwenye hafla hiyo.

Katika mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika mkoani Kilimanjaro, Machi mwakani, mshindi wa jumla atajinyakulia kitita cha shilingi milioni nne na ushindi huo ukienda kwa Mtanzania ataongezewa milioni moja na nusu hivyo kupewa milioni tano na nusu.

Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akielezea dhumuni la kampuni yake kudhamini mashindano hayo.
Rais wa Chama Riadha nchini (RT) Anthoni Mtaka naye akitia neno.
Waziri Mwakyembe, wadhamini na viongozi baada ya kuzindua mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini, Leodgar Tenga naye alitia neno.
Picha ya pamoja mgeni rasmi akiwa na viongozi na wadhamini wa mashindano hayo.

 

PICHA: RICHARD BUKOS /GPL  

Comments are closed.