The House of Favourite Newspapers

Waziri Nape Aibuka na Crew, Leaders Kwenye Shoo Usiku

WAZIRI wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo ikiwa ni shehemu ya kuhamasisha sanaa na kuonesha mfano kwa viongozi wengine wa serikali kuusapoti mziki wa Bongo Fleva, usiku wa kuamkia leo Februari 19, 2017, aliibuka kwenye Viwanja vya Leaders Club ambako kulikuwa na shoo baab kubwa iliyokuwa ikiwakutanisha vinara wa RnB hapa Bongo, ambao ni Juma Jux, Ben Pol pamoja na Barakah da Prince.

Nape aliibuka viwanjani hapo majira ya saa 4:00 akiongozana na crew yake na mara baada ya kuwasili kama ilivyo ada alipita kwenye zuria jekundu (red carpet) na kufotolewa picha kadhaa na wanahabari kisha kuzama ukumbini kwa ajili ya kushuhudia shoo hiyo.

Nimekuwekea picha tatu za Waziri Nape alivyoibuka kwenye shoo hiyo.
Shoo ilikuwa ya ukweli… cheki Full Video hapa.

PICHA NA MUSA MATEJA | GLOBAL TV ONLINE

Comments are closed.