The House of Favourite Newspapers

WAZIRI ULEGA AFUNGUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SIKU YA UKIMWI

0
Waziri Ulega akipata elimu ya maambukizi ya ukimwi kwenye moja ya mabanda aliyotembelea.
Mwananchi (kulia) akipewa ushauri na daktari baada ya kupimwa.
Wananchi wakitembelea mabanda yanayotoa huduma mbalimbali uwanjani hapo.
Moja ya mabango yaliyokuwepo.
Sehemu ya watu waliohudhuria tukio hilo.
Unga wa lishe ulikuwa ukiuzwa kwa ajili ya kuboresha afya.
Moja ya mabanda ya upimaji virusi vya ukimwi likiwa tupu kutokana na idadi ndogo ya watu waliofika kupima.
Ulega akionyesha vitabu baada ya kuzindua kitabu cha mkakati wa taifa wa kondomu.

 

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega, leo Jumatatu alimwakilisha Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama. kwenye uzinduzi wa wiki ya siku ya Ukimwi duniani ambapo alikabidhiwa maboksi matatu yenye mipira ya kiume (kondomu) kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya maradhi hayo.

Ulega alikabidhiwa zana hizo katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo kilele chake kitakuwa Desemba 1 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu.

Katika uzinduzi huo Ulega aliyatembelea mabanda yaliyokuwa yakitoa huduma mbalimbali za masuala ya ukimwi ukiwemo upimaji, nasaha, lishe bora na mengineyo ambapo alipokea maelezo kutoka kwa wahusika.
Baada ya kutembelea mabanda hayo waziri huyo alitoa hotuba ambapo kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya kwa sasa maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua kwa kiasi kikubwa na kufikia mwaka 2030 maambukizi hayo yanatakiwa kutokomezwa kabisa.

Alisisitiza kwamba kinga ya mipira ya kiume na kike inasaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo aliwataka wananchi wote kuwa anayeshindwa kujizuia kufanya ngono atumie kinga hiyo.

Amewaonya ‘wanaotembea pekupeku’ kwani wanapopata maambukizi serikali inapata gharama kubwa ya kuagiza madawa nje ya nchi kwa ajili ya kutibu magonjwa yanayosababishwa na virusi hivyo.
Baadaye Ulega alizindua kitabu cha maambukizi ya ukimwi ambapo baada ya kukizindua alikabidhiwa maboksi matatu yenye kondomu.

Wakati akipokea maboksi hayo waziri huyo alisema kwake kutumia mipira hiyo siyo kwa ajili ya kufanya ngono isipokuwa kwa ajili ya uzazi wa mpango.

NA RICHARD BUKOS/GPL

 

Leave A Reply