The House of Favourite Newspapers

Wazungu Wajitokeza Kujenga Uwanja Yanga SC

0

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa tayari umepata kampuni itakayojenga Uwanja wao Kigamboni jijini Dar, huku ikidaiwa kuwa ni kampuni kutoka Ulaya.

 

Yanga wapo kwenye mchakato wa kujenga uwanja wa kisasa eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na tayari walishatangaza tenda na imepata mwenyewe.

Yanga chini ya uongozi wa mwenyekiti wake, Dk Mshindo Msolla, iliweka mikakati ya kuhakikisha timu hiyo inamiliki uwanja wa kisasa utakaoendana na hadhi ya timu hiyo. Akizungumza na Championi Jumatano, Ofi sa Mhamasishaji wa timu hiyo, Antonio Nugaz alisema kuwa tayari wapo katika mazungumzo na kampuni moja ambayo imejitokeza kwa ajili ya tenda hiyo ya uwanja na mazungumzo yanazidi kuendelea.

 

“Tayari uongozi wa Yanga upo kwenye mazungumzo na kampuni moja ambayo imeonyesha nia ya kuhitaji kutujengea uwanja wetu wa kisasa ambao tutautumia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zetu zote za kimichezo.

 

“Yanga ni kubwa sana na moja ya mikakati katika uongozi wetu ni kuhakikisha tunajenga uwanja wa kisasa
utakaotumika kuendesha shughuli zetu zote za kimichezo.

 

“Hapo awali tulitangaza tenda hiyo, hivyo hata katika masuala ya ujenzi itakuwa ni faida kubwa sana kwa Wanayanga kwani naamini kupitia ujenzi huu wengi sana watapata kazi, hivyo ni fursa kwao na wakae mkao wa kula,” alisema kiongozi huyo.

 

Hata hivyo, Nugaz hakusema kuwa kampuni hiyo inatoka wapi lakini chanzo kilisema kuwa ni kutoka Bara la Ulaya.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave A Reply