The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Aibuka Upya Instagram

wema-2

MREMBO asiyeishiwa matukio kila kukicha Bongo, Wema Isaac Sepetu hatimaye ameibuka kwa mara nyingine Instagram baada ya kuitelekeza akaunti yake kwa muda ambapo alifuta picha zake zote za zamani na kubakiza maswali mengi kwa mashabiki wake ambao hawakuweza kupata majibu.

Kabla ya kufuta kila kitu kwenye akaunti yake hiyo, Wema alikuwa na zaidi ya followers milioni mbili na nusu, ambao wameendelea kumvumilia hadi jana jioni aliporejea na kuanza kuweka picha mpya kwenye profile yake kisha akaipost upya kwenye akaunti yake hiyo.

wema-1

Hadi muda huu, Wema bado hajatoa sababu ya msingi iliyomfanya aamue kufuta posti zake hizo pamoja na kuwa na maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimtaka awafafanulie kilichomfanya kuchukua uamuzi huo.

Wema ameandika yafuatayo kwenye akaunti yake:

Happy 2017… and am excited.. how Many Likes?? Share from
This one and am gonna Tell You something to Celebrate for the whole Year…. #WSSoCloseToYou #WSladieschoice #WSyourAddiction
#unataka kusikia jambo zuri kutoka kwangu kwa mwaka 2017? Gonga Likes za kutosha and nitarudi kukung’ata sikio… This be your First Image…. There is plenty of these Just for You…. I missed You too…. @ossegrecasinare You are Life….

Comments are closed.