Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge.
Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku.
Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na Shemeji wa marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.
Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye alikuwa Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian
Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo
Waombolezaji wakiwa kwenye msiba.
Jirani rafiki wa karibu wa marehemu, Mpoki, maarufu kwa jina la Mijisu akilia wakati wa msiba
Comments are closed.