The House of Favourite Newspapers

Wengi Wanaachika kwa Kutikisa Kiberiti, Jifunze!

Na ERICK EVARIST |RISASI JUMAMOSI| LOVE STORY

MWANAMKE wangu ukimuambia naomba uwe unazima friji kwa kipindi ambacho halina ulazima, huwa anajaribu kuliacha ili aone nitamfanya nini. “Anatikisa kiberiti. Anapuuza makusudi, nikiliona friji linaunguruma na wakati huo hakuna ulazima wa kuliwasha, nikimuuliza kwa nini umeliacha, ananiambia nilisahau. “Mimi nalizima. Namueleza kwamba anapaswa kuwa makini sababu ya kubana matumizi. Kesho tena unakuta ameacha hivyohivyo, ukimueleza anakwambia ‘kwani si ulizime wewe kama umeliona, hadi nizime mimi?’

“Namueleza kwamba asifanye hivyo, hali ya uchumi ni ngumu na mlipaji ni mimi, siku nyingine asifanye hivyo halafu nalizima. Unakaa siku mbili tatu, tatizo lile tena linajirudia. “Unakwenda kwenye shughuli zako, ukirudi unakuta friji linaunguruma tena kutwa nzima kukiwa hakuna kitu chochote kilichowekwa ndani yake. “Jambo hili sio kwenye friji tu. Hata KWA KUTIKISA Wengi wanaachika KIBERITI, JIFUNZE!
kwenye vitu vidogovidogo. Wakati mwingine, namuambia ajitahidi akichana nywele zake kwa kitana ambacho natumia, ahakikishe anatoa nywele zinazobaki kwenye kitana, anaziacha tu makusudi. “Anafanya hayo yote kama kutikisa kiberiti.

Anajaribu kunitunishia msuli. Akiona nimemaindi, anashuka. Anakuwa mpole. “Yaani kuna ukorofi huwa nauona kama vile huwa anaamua tu kuufanya.

Unamuachia nguo na kumwambia azifue mwenyewe, asimuachie dada wa kazi kwani amekuwa akikosea kufua vile ambavyo unataka. Anakusikiliza leo, kesho ukirudi unamkuta dada wa kazi anafua. Nakasirika kwelikweli. “Sasa kuna wakati niliamua kumuonesha sura ya kukasirika na kumkemea kwa hasira katika kila jambo, aliliacha mara moja. Nikamwonesha kwamba nimekasirika, kwa kila jambo nilimwambia kama ataendelea nalo, nitamfanyia kitu ambacho hatakisahau maishani,” huo ni mfano kutoka kwa msomaji wangu. Karibu tujifunze sasa;

SOMO KWA WANAWAKE Kuna wanawake wana kasumba ya namna hiyo. Wanapenda kuwajaribu wenzi wao katika mambo fulani ili kuona watafanya nini. Akiambiwa usifanye hivi, yeye anafanya. Akiona umenyamaza, hujaonesha kumkaripia, kesho anarudia. Yaani anafanya ilimradi tu. Anataka kuona utakasirika kiasi gani. Unamwambia naomba uniwekee maji ya kuoga, anakwambia nenda kaweke mwenyewe.

Au anakupa yale majibu ya ‘mimi mwenzako nimechoka’. Anaambiwa na mumewe, nipigie pasi majibu yake ni ‘kapige mwenyewe. Na mimi huwa nachoka’ HILI NI TATIZO!

Mwanamke anapofanya hivyo, anasababi sha ugomvi wa mara kwa mara na kuamua kumuacha mwanamke wa aina hiyo bila hata ya kumuambia nini tatizo lake. Wanaume wengi wanakutana changamoto hiyo.

Wapo wanaoweza kutenda kwa kumchimba mkwara mwenzi wake na kufanikiwa kunyoosha mambo lakini wengine wanaamua kufanya maamuzi yao moyoni. Anabwanga manyanga chini, anaendelea mbele. Wanaume wanapofanyiwa mambo hayo huwa wanaamini wamedharauliwa.

Unapomfanyia jambo ambalo anaona unaweza kulifanya anaudhika mno. Anajenga ile dhana ya yeye ni kichwa cha familia. Anakasirika kuona kwenye eneo hilo anashindwa kuheshimika hata kama ni jambo dogo kiasi gani lakini linaweza kuleta madhara makubwa ambayo yanaweza kugharimu kabisa uhusiano wenu. Kwenye akili yake anafikiri, usipomheshimu yeye utamheshimu nani? Amekueleza usifanye hivi kwa sababu unamkera, unafanya halafu unasikilizia.

Mungu asaidie aamue kukuchimba mkwara na wewe ufanye. Au akuseme halafu mgombane, muachane.

INAKUGHARIMU NINI KUTII?

Nimeshawahi kusema kwenye makala zangu huko nyuma, kuna gharama gani mke akimtii mumewe katika mambo ambayo hayana gharama yoyote kwake? Utapungukiwa nini? Ukimtii mumeo unayemfahamu kwamba ndiye kichwa cha familia?

JIFUNZE KWA MAANDIKO HAYA!

“Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo,” Waefeso 5: 21-23. Sasa

Save

Comments are closed.