The House of Favourite Newspapers

WHO Yaomba Takwimu za Corona Tanzania

0

 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema shirika lake halijapokea taarifa kutoka #Tanzania kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhusiana na #COVID19.

 

 

Tedros amesema hali hiyo inatia wasiwasi na ametoa wito kwa Serikali ya Tanzania kuanza kuratibu maambukizi na kutoa data kuhusiana na COVID-19 nchini humo.

 

 

Tedros amesema mwishoni mwa Januari alishirikiana na Mkuu wa WHO barani Afrika, Matshidiso Moeti, katika kuihimiza Tanzania kuongeza hatua za kiafya dhidi ya COVID-19 na kujiandaa na mikakati ya kutoa chanjo.

Leave A Reply