The House of Favourite Newspapers

William Malecela ‘Lemutuz’, Mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani Afariki Dunia

0

Mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, John Malecela, William Malecela almaarufu Lemutuz, amefariki dunia asubuhi ya leo, Mei 14, 2023.

Taarifa za kifo cha Lemutuz, zimethibitishwa na meneja wa Lemutuz Online, Deusdedith Innocent, @deustanzania.

Lemutuz aliyekuwa mmiliki wa kituo cha habari za mitandaoni, Lemutuz Superbrand, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Aamin.

Leave A Reply