The House of Favourite Newspapers

Wimbo wa Roma Kutengenezewa Filamu

0

DAR: Wimbo wa Mkombozi wa mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ ambao amemshirikisha msanii One Six, unatarajiwa kufanyiwa filamu.

Wimbo huo umetengenezwa kwenye Studio za Tongwe chini ya Prodyuza J Murder ambao ndiyo wimbo aliofungua nao mwaka 2020.

Roma ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, anajiandaa kufanya filamu ya wimbo huo ambao umejitosholeza kwa sababu uko kwenye audio na video na sasa unakuja kwenye filamu.

“Tunajaribu kufanya projekti fulani ya tofauti kabisa ndiyo maana nimetengeneza huo wimbo na ninaufanyia filamu kabla ya ziara ya kiumuziki nitakayoianza hivi karibuni,” amesema Roma.

Stori: Neema Adrian, Ijumaa

Leave A Reply