The House of Favourite Newspapers

Wizara ya Afya Yanuia Kuongeza Kasi ya Matumizi ya Chanjo ya Uviko-19

0
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu leo Juni 02, 2022 amezindua zoezi la kuongeza kasi ya matumizi ya chanjo ya Uviko 19 katika Viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar.

 

Waziri Ummy amesema kwa sasa dunia inapitia wimbi la nne la ugonjwa wa Uviko-19 huku Tanzania ikiwa inachukua hatua katika kila ngazi ya mabadiliko ya ugonjwa huo.

 

Akiongea na wananchi katika Hotuba yake Waziri Ummy amesema njia pekee ya kujikinga na madhara ya ugonjwa huu ni kuchanja hivyo amewaasa wananchi kuchukua hatua madhubuti za kuchanja.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright

Waziri Ummy amebainisha kuwa katika kipindi cha wiki tatu zilizopita kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa Uviko-19 hususan nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara hasa nchi za Kusini mwa Afrika.

 

Waziri wa Afya amesema kuwa nchi ya Afrika Kusini imeripoti visa vipya vya Uviko-19 zaidi ya laki mbili katika kipindi cha wiki tatu zilizopita huku nchi jirani ya Kenya nayo ikiripoti ongezeko jipya la wagonjwa ambapo sasa kutokana na muingiliano wa shughuli za kibiashara Tanzania nayo inajipanga katika kukabiliania na wimbi la tano la ugonjwa huo huku njia sahihi ikiwa ni wananchi kuchanja chanjo ya Uviko-19

 

Naye BaloziĀ  wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright amesema Serikali ya Marekani inapanga kuongeza kiasi cha Dola milioni 300 kama msaada kwa nchi ya Tanzania ili pesa hizo ziweze kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Uviko-19.

 

Waziri Ummy Mwalimu ametoa tathmini kuwa tangu zoezi la Kuchanja lianze jumla ya watanzania milioni nne na laki sita ambayo ni sawa na 15.2% ya wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamefanikiwa kupata chanjo ya Uviko-19.

Leave A Reply