The House of Favourite Newspapers

Wizara Ya Nishati Yazindua Umoja Wa Wazalishaji Na Wasambazaji Wa Gesi Ya Kupikia Majumbani

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akitaka utepe kuashiria uzinduzi huo.

Dar es salaam: 15 Machi 2023, Wizara ya Nishati Yazindua Umoja wa Wazalishaji na Wasambazaji wa Gesi za kupikia majumbani maarufu kama LPG.

Akizindua umoja huo kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema;

“Sisi kama Wizara ya Nishati na Serikali tunachokisema ni kwamba, kuanzishwa kwa umoja huu wa wasambazaji wa gesi ya kupikia majumbani kwanza kutarahisisha mawasiliano kati ya makampuni haya na serikali.

Shangwe baada ya uzinduzi huo.

“Kwasababu sasa serikali itakuwa inahusiana na umoja huu, lakini pia tunasema ya kwamba wasambazaji hawa wa gesi ya kupikia majumbani wanachangia kwenye maono ya mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kama alivyoyaezea kinaga ubaga katika mkutano au majadiliano ya jinsi ya kuhama kutoka katika nishati chafu kwenda nishati safi ya kupikia katika mkutano uliofanyika tarehe moja na mbili Novemba mwaka jana 2022.

Mgeni rasmi na wadau wakiangalia skrini iliyokuwa ikisherehesha uzinduzi huo.

“Katika mkutano huo Mheshimiwa Rais alisema angependa kuona katika miaka kumi ijayo asilimia 80 ya Watanzania wanapikia nishati safi.

“Lakini pia alisema kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja yaani mpaka mwezi Januari mwakani taasisi zote ambazo zinalisha watu zaidi ya 300 ziache kutumia kuni na mkaa na kuja kwenye vyanzo vingine vya nishati ya kupikia kama LPG na nishati nyingine.

Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

“Kwahiyo leo hii tunapozindua umoja huu wa wasambaji wa nishati safi ya kupikia ni sehemu ya kutimiza maagizo ya mheshimiwa Rais ya kwamba sekta binafsi ishirikishwe kikamilifu katika kuleta majawabu ya nishati safi ya kupikia hapa nchini.

“Na hivyo leo hii kukata utepe na kuzindua umoja huu ni ishara ya kwamba sekta binafsi sasa imeamka na iko tayari kushirikiana na serikali katika kutekeleza azma hii ya kuahakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia”. Alimaliza kusema Mhandisi Felchesmi. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS/ GPL

Leave A Reply