The House of Favourite Newspapers

Wizara ya sheria Marekani yasema Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushtakiwa

0

Wizara ya sheria ya Marekani imesema Rais wa zamani Donald Trump anaweza kushtakiwa na maafisa wa Polisi wa bungeni waliojeruhiwa na wabunge Wademokrat juu ya uasi wa Januari 6, 2021 katika bunge la Marekani.

Msimamo wa wizara hiyo kwamba Trump hana kinga kutokana na kesi kama hizo ilibainika katika kesi iliyowasilishwa kwenye mahakama ya rufaa ya serikali kuu iliyotolewa Alhamisi.

Maelezo hayo yaliwasilishwa na mawakili katika Kitengo cha kesi zisizo za jinai cha wizara ya sheria na haihusiani na uchunguzi tofauti wa kijinai unaofanywa na mwendesha mashitaka maalum wa wizara hiyo ili kujua ikiwa Trump anaweza kushtakiwa kwa mashitaka ya jinai kwa juhudi za kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 katika ghasia za bungeni.

ROSE MUHANDO ATUMA UJUMBE KWA MWANA FA”BASATA MMETUWEKA NA HUKO KWINGINE MUTUWEKE”#Mtoko wa pasaka

Leave A Reply