The House of Favourite Newspapers

Feisal Ni Mali Ya Yanga, TFF Wakomalia Maamuzi Ya Awali, Yatupilia Mbali Shauri – Video

0

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana Machi 2, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Young Africans kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Young Africans.

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali na hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

Leave A Reply