The House of Favourite Newspapers

Wizi ulinikosanisha na Joh Makini

0

Boniphace Ngumije

DE Fatality International ni ‘label’ ya muziki maarufu Bongo iliyo chini ya jamaa anayefahamika kwa jina la  Jerry Boniphace ‘Mensen Selekta. Nimegonga naye stori mbili tatu kuhusu game na hiki ndicho alichofunguka;
Showbiz: Watu wamekufahamu sana kupitia u-prodyuza lakini sasa unaimba, kwa nini uliamua kuimba?
Mensen: Ni kitu ambacho kiko damuni, nimeanza kuimba long time.

Showbiz: Mpaka sasa umefanya kazi na wasanii wa nje wangapi?
Mensen: Wasanii wa nje wapo wengi, baadhi yao tu ni Eppsod wa Ghana, Naazizi wa Kenya, Cash Mare kutoka Marekani.
Showbiz: Kuna tetesi ziliwahi kuenea kwamba ulimtumia Rick Ross mdundo kwa ajili ya kupiga naye kazi, kuna ukweli wowote juu ya hili?
Mensen: Yaa ni kweli lakini iko hivi; kuna Dj maarafu Marekani anaitwa DJ Ill Willy, huyu huwa anaandaa ‘project’ na wasanii wa kimataifa na kufanya nao ‘mixtape’. Amekwishafanya na Chris Brown, DMX na wengine wengi.

Sasa huyu jamaa aliwahi kutangaza kwenye tovuti yake kuwa prodyuza mkali anayeweza kuandaa mdundo unaomfaa Rick Ross afanye hivyo kisha atume. Mimi nililiona hilo tangazo nikafanya mdundo na kuutuma ambapo baadaye nikaambiwa nilishinda. Ikaandaliwa project lakini sikujua iliishia wapi.

Showbiz: Kuna project nyingine yoyote ya kimataifa umewahi kufanya?
Mensen: Ndiyo, inaitwa Ray Of Hope. Hii ni project ambayo hufanyika kila mwaka na husimamiwa na Umoja wa Mataifa (U.N). Sasa mwaka 2013, project iliandaliwa na Rais Mstaafu wa Izrael, Shimon Peres na kutoka Tanzania ni mimi niliyepata nafasi ya kushiriki kwenye wimbo huo.

Showbiz: Kuna utata juu ya prodyuza aliyeandaa Ngoma ya Izzo Business iitwayo Riz One, Nahreal huwa anasema ni yeye, wewe kwenye ‘wikpedia’ yako umeandika kuwa ndiye uliyeandaa, hebu tatua utata.

Mensen: Ni kweli kuna makosa yalifanyika. Kuna mshkaji wangu alikuwa anaitwa Shoa Kizzy (Sasa marehemu) huyu ndiye aliandika katika wikpedia yangu. Kwa kuwa nilikuwa karibu na Izzo na ndiyo ikawa sababu ya yeye kufikiri wimbo huo niliuandaa mimi.

Akauandika kwenye wikpedia lakini kabla sijashtukia lolote mshkaji alifariki nikiwa bado sijajua password.
Showbiz: Nini ilikuwa sababu ya kuzinguana na Joh Makini?
Mensen: Kwa kifupi niligombana naye kwa madai ya wizi, kwamba kuna ‘idea’ niliichukua kutoka kwake na nikampa msanii mwingine, lakini ishu hiyo ilikwisha kitambo.

Leave A Reply