The House of Favourite Newspapers

Wolper Achimba Mkwara Mzito

0

MWANADADA anayekiwasha kunako Bongo Movies, Jacqueline Wolper Massawe ambaye ni mjasiriamali mkubwa amechimba mkwara mzito.Wolper ametoa onyo kali kwa wale wanawawake wanaopenda kuchukua wanaume za watu.

 

Akizungumza na IJUMAA WIKIENDA, Wolper anasema kuwa mtu atakayemchukua mpenzi wake wa sasa ambaye ni mbunifu wa mavazi, Rich Mitindo watagawana majengo ya Serikali; mmoja apelekwe mochwari Muhimbili na na mwingine aende jela Segerea.

 

“Kwa kuwa niliamua mwenyewe kwa moyo wangu kuwa na Rich, sihitaji tena kuacha wala kuachwa na huyu. Sasa hivi ni hama zangu ama zake kwa wanawake wanaojifanya wenyewe wapo mjini kwa ajili ya waume za watu; yaani tutabadlishana majengo ya Serikali,” anasema Wolper ambaye ni muuza vitenge maarufu jijini Dar.

Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply