The House of Favourite Newspapers

HATARI: Panya Road Wazua Balaa Dar, Mtu Mmoja Afariki – VIDEO

Wakati matukio ya vijana wadogo maarufu kama Panya Road kuvamia na kujeruhi watu yakiwa yameanza kusahaulika, tukio jipya limeibuka Ulongoni, Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

 

Katika tukio hilo, vijana hao wahalifu maarufu kama Panya Road, waliwavamia, kuwapora, kuwakata mapanga, kuwachoma bisibisi wakazi wa maeneo hayo huku pia wakiwadhalilisha wanawake na kibaya zaidi, uhalifu huo ukasababisha Hussein Kikomaga mwenye umri wa miaka 28 kufariki dunia.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda, kundi hilo lilianza kufanya uhalifu huo kuanzia majira ya saa moja usiku ambapo walianza kuwapora na kuwashambulia wakazi wa eneo hilo huku wakiwadhalilisha wanawake.

 

Shuhuda huyo aliendelea kudai kuwa, kundi hilo liliwajeruhi watu wengi ambapo lilifika mpaka eneo la kibao cha Shule ya Ulongoni ambapo marehemu alikuwa ndipo kwenye ofisi yake ya ufundi wa pikipiki.

VIDEO: TAZAMA UJIONEE MWENYEWE HAPA

Comments are closed.