The House of Favourite Newspapers

Wolper akivishwa pete tu kwisha habari yake!

IMG-20150310-WA0054Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper.

KUMBE! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta wa kuwa naye maishani yaani mke au mume.

Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaweza kuthibitisha hilo baada ya uchunguzi kuonesha kuwa ana listi ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka, wakaingia mitini.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakitumia gia hiyo kumrubuni na kumwachia maumivu makali ya moyo.

Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha kabisa kwa wazazi lakini baada ya kumfaidi wakammwaga na kujikuta akihamia kwa mwingine, jambo ambalo watu wengine ambao ni mashabiki wake wamekuwa wakihoji ana nini mpaka yamkute hayo?

ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’
Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya uchumba na kumtambulisha mpaka kwa wazazi wake naye kujitambulisha kwa wazazi wa mwanadada huyo lakini walimwagana baada ya Wolper kuhisi kwamba anasalitiwa kwa mpenzi wake huyo kuwa na uhusiano na wasanii wenzake.

Dallas alikuwa akimpa Wolper fedha za kutosha ambapo kipindi hicho aliweza kumchangia msanii mwenzake ambaye ni marehemu kwa sasa, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kiasi cha Sh. milioni 15 kwa ajili ya matibabu nchini India huku katika kumbi mbalimbali za starehe akitunza kama hana akili nzuri.

wolper-4GEE MODO
Jamaa huyo ni mfanyabiashara anayemiliki maduka ya viatu na nguo maeneo ya Kinondoni jijini Dar ambapo baada ya Wolper kuachana na Dallas naye aliingia kwa gia ya kumvisha pete ya uchumba na mapenzi kuwa motomoto kwa kile kilichoonekana kwamba anampooza machungu.

Hawakukaa muda mrefu, wawili hao waliachana japokuwa sababu za kumwagana kwao hazikujulikana ila tayari jamaa huyo alikuwa ameshamfaidi Wolper.

JIMMY MGAYA
Jimmy ni Mbongo aishiye Afrika Kusini ‘Sauz’ ambaye naye ni mfanyabiashara pia. Baada ya Wolper kuachana na Gee Modo alinasa kwa Jimmy ambapo kwa mara ya kwanza zilinaswa picha zao za kimahaba wakiwa nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba, kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huo haukudumu kwa muda mrefu ukavunjika.

MWAMI RAJABU
Mwami ni mfanyabiashara wa madini ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mara nyingi Mwami hupatikana jijini Dar kwa kazi zake za kibiashara ambapo hufikia hoteli za kifahari.

Mwami anatajwa kwamba aliwahi kumvisha pete ya uchumba Wolper lakini hakuna kilichoendelea baada ya jamaa huyo kudaiwa kupata alichokitaka.

Wolper na Mwami walianzisha uhusiano ambapo mwanadada huyo alikuwa na fedha za kumwaga lakini waliachana huku sababu zikiwa hazijulikani, japokuwa mfanyabiashara huyo anadaiwa kuwa na uhusiano na mastaa mbalimbali wa Bongo baada ya kuachana na Wolper.

MKONGO
Katika kujaribu tena bahati yake, Wolper aliingia kwa Mkongo mmoja ambaye mpaka wanaachana jina lake halikupatikana. Kama ilivyokuwa kwa wengine, uhusiano huu haukuchukua muda mrefu na kuvunjika.

Mkongo huyo alimvisha Wolper pete ya uchumba na alikuwa akisema mara kwa mara kuwa wapo kwenye mipango ya ndoa hata pale ukweli ulipogundulika kwamba ni mume wa mtu ambapo Wolper alidai atakomaa mpaka mwisho wa siku wakaja kumwagana baada ya Mkongo kumfaidi mrembo huyo.

Comments are closed.