The House of Favourite Newspapers

Wosia kifo cha Jokate

0

Stori: Brighton Masalu na Boniphace Ngumije

UCHURO? Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ ametabiri kile kinachoweza kuitwa ‘wosia wa kifo chake’ kwa kuweka wazi mazingira ambayo angependa yafanyike siku atakapotangulia mbele ya haki.

MAJENEZAYAJIDEAkizungumza na gazeti hili juzi, mmoja wa rafiki wa Jokate (jina tunalo), alisema staa huyo anapenda msiba wake uwe na mazingira yanayoendana na hadhi yake ikiwemo jeneza lililopambwa kwa vito vya thamani na kaburi zuri.

“Ishu ya atazikwa wapi anaiachia familia yake. Lakini anapenda siku ya kuagwa aagwe kistaa (Leaders), watu wengi wajitokeze,” alisema rafiki huyo.

Jokate ambaye ni Miss Tanzania Na. 2, 2006 pia mkurugenzi wa nembo ya Kidoti inayojishughulisha na urembo na mitindo, anadaiwa amekuwa akijiuliza namna itakavyokuwa siku atakapoaga dunia. Wakati mwingine anatamani angekuwa na uwezo wa kushuhudia.

Amani lilimtafuta Jokate kwa njia ya simu na alivyopatikana alisema ilivyoelezwa ndivyo angependa iwe na kwamba hakuna binadamu anayetamani msiba wake uwe wa ajabu.

“Yeah! Mimi ni mtu wa watu, hadhi yangu kwenye jamii unaijua, japokuwa ukweli unabakia kwamba muhimu ni matendo mazuri, lakini hata hadhi ya mazingira ya msiba iwe nzuri kulingana na utu.

“Napenda jeneza zuri, nyumba nitakayopumzishwa (kaburi) iwe nzuri ili ibaki kumbukumbu kwa kizazi kijacho kuwa Jokate aliishi akafanya hiki na hiki. Napenda watu wote wahudhurie, mimi ni mtu wa watu. Ila wapi nizikwewazazi wangu wataamua,” alisema Jokate kwa sauti ya utulivu.

Leave A Reply