The House of Favourite Newspapers

Xabi Alonso Athibitisha Kubaki Bayer Leverkusen

0

KOCHA wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso amethibitisha kuwa atabaki klabuni hapo licha ya fununu zinazoendelea kumhusisha na kuondoka huku vilabu vya Liverpool, Bayern Munich na Real Madrid vikitajwa kuhitaji huduma yake.

Akizungumza Machi 29, 2024 kwenye mkutano na waandishi wa Habari Xabi amesema amekutana na kufanya mazungumzo na Waajiri wake hao na kuwaambia kuwa atabaki na kuendelea kuwatumikia vinara hao wa Bundesliga.

“Baada ya tetesi nyingi juu ya mustakabali wangu nimetumia mapumziko ya kimataifa kutafakari na kufanya maamuzi. Hapa ni mahali ambapo natakiwa kuwepo.” amesema Xabi.

Kiungo huyo wa zamani wa Real Sociedad, Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich amekuwa na wakati mzuri ndani ya Bayer Leverkusen akiiongoza klabu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga ambapo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa msimu huu kwenye michuano yote.

Leave A Reply