The House of Favourite Newspapers

Ya Snura yamkuta Gigy money!

0

stori:  hamida hassan na Gladness mallya, Ijumaa
DAR ES SALAAM: ZIKIWA ni siku chache zimepita tangu staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi kufungiwa video yake ya Chura na kutakiwa kuitengeneza upya, Video Queen, Gift Stanford ‘Gigy Money’ (pichani) naye amejikuta akikumbana na rungu la Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kufuatia kusambaza kava la video ya wimbo wake mpya lenye picha yake inayomuonesha akiwa mtupu.
Kava hilo la wimbo wake wa Supu ambao alitarajia kuuachia jana, alilisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambapo mashabiki walioiona kwa mara ya kwanza walishangazwa na kitendo hicho kwani picha yake haikumstiri mwili kama yalivyo maadili ya Kitanzania.

“Yaani hawa wasanii ni sikio la kufa, Gigy ameweka kava hili ambalo lina picha yake ya nusu utupu kabisa na limesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, hajajifunza kwa mwenzake Snura?” alihoji mdau mtandaoni.

Walipotafutwa Basata na kuulizwa juu ya video queen huyo, Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza alisema wao wanasimamia maadili ya Kitanzania hivyo kama Gigy amekiuka, wanampa onyo asiuachie wimbo huo hadi atakapoufanyia marekebisho.

“Kwanza huyo Gigy Money hatumtambui kabisa hapa baraza maana hajajisajili kama msanii na sheria ya mwaka 1984 inasema mtu yeyote hatakiwi kufanya kazi ya sanaa bila kujisajili hivyo hata hao ma-video queen wanatakiwa wajisajili maana hatuwatambui.

“Mtu akikiuka maadili, hatumvumilii na asitegemee kazi yake kupigwa katika vyombo vya habari wala mitandao, tunawasihi wasanii kutoa kazi zenye maadili ili kuepuka usumbufu,” alisema Mngereza.
Alipotafutwa Gigy kuhusiana na suala hilo, alisema:
“Mimi najua ma-video queen hatuhusiani na mambo ya Basata na niseme tu wimbo wangu wuko ndani umetulia, kava lisiwatishe ila nitaenda Basata kufuata utaratibu,” alisema Gigy.

Leave A Reply