Yacouba Atua Tunisia, Apewa Daktari Bingwa
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Injinia Hersi Said, amesema kuwa kiungo wao mshambuliaji Mburkinabe, Yacouba Songne, anaweza kupona haraka na kurejea uwanjani kutokana na uhodari
wa daktari Mtunisia atakayemtibu majeraha yake.
Yacouba alipata majeraha ya goti katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Majeraha huyo yalimsababishia ashindwe kumalizia mchezo huo wa kirafiki katika kipindi cha kwanza cha mchezo
huo na nafasi yake kuchukuliwa na Mrundi, Said Ntibazonkiza ‘Saido’.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Said alisema kuwa mshambuliaji huyo tayari amefika Tunisia salama
akiwa ameambatana na daktari wa timu hiyo, Youssef Mohamed na haraka ataanza kupatiwa matibabu.
“Yacouba ameondoka nchini jana (juzi) kuelekea Tunisia ambako amekwenda kwa ajili ya matibabu ya
goti lake aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Ruvu.
“Amekwenda kupatiwa matibabu nchini humo baada ya kujiridhisha kupitia watalaamu wetu kwamba
kuna daktari bingwa ambaye atamaliza tatizo lake.
“Ndani ya Yanga hivi sasa tuna daktari wa viungo bora ambaye amefanya kazi nchini Tunisia, Youssef (Ammar)
katika klabu kubwa za pale na akishirikiana na kocha wetu, hivyo wametuthibitishia daktari ambaye
atakwenda kumtibu Yacouba atamaliza tatizo lake,” alisema Said.
Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam | Championi Ijumaa