The House of Favourite Newspapers

Yaliyojiri Kortini Kesi ya Mwakabibi

0

KESI inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam Lusubilo Mwakabibi na mwenzake Edward Haule ambaye alikuwa mratibu wa mradi wa DMDP, imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hadi Septemba 30, 2021 kutokana na upelelezi kutokamilika.

 

Mwakabibi na mwenzake Haule wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo kwa mara ya kwanza walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi, ambapo Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanakombo Rajab alisema katika kosa la kwanza watuhumiwa wote wawili wanashtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kuelekeza ujenzi wa stendi ya mabasi katika kiwanja kinachomilikiwa na Kanisa la Angilikana bila ya kupewa ruhusa, kosa waliolitenda kati ya Machi 2020 na 2021.

 

Katika kosa la pili, washtakiwa hao wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya kwa makusudi kinyume cha kifungu cha 3 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria ya Ardhi.

 

Upande wa utetezi ukiongozwa na Jeremiah Mtobesya umeomba upande wa mashtaka kukamilisha uchunguzi mapema na endapo wakigundulika hawana hatia waachiwe huru wakaendelee na majukumu yao.

Leave A Reply