The House of Favourite Newspapers

Yaliyojiri Kortini Kesi ya Nabii Tito Kutaka Kujiua

KESI ya kujaribu kujiua kwa kujichana tumbo na wembe inayomkabili mshtakiwa Onesmo Machibya maarufu Nabii Tito, imeahirishwa katika Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma hadi  Machi 19, 2018.

 

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha aliagiza mtuhumiwa huyo kuchukuliwa vipimo vya akili katika Taasisi ya Magonjwa ya Akili ya Isanga, Dodoma ili kubaini iwapo  ana matatizo hayo.

 

Mtuhumiwa huyo (Nabii Tito) hakufika mahakamani leo ambapo kesi yake iliahirishwa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, James Karayemaha kutokuwepo mahakamani.

 

Nabii Tito alifikishwa kortini kwa mara ya kwanza Januari  29, 2018 na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua kwa kujikata na wemb ambapo anadaiwa kufanya tukio hilo Januari 25, 2018 wakati akiwa mahabusu.

UNDANI Kuhusu Mtanzania Aliyeuawa Afrika Kusini

Comments are closed.